Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, wanazuoni wa kidini wamekubali mwaliko wa Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Sheikh Ali al-Khatib, Naibu Raisi wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon, kwa ajili ya mkutano huu.
Mkutano huo wa wanazuoni umefanyika katika makao makuu ya Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia katika barabara ya uwanja wa ndege, kwa mwaliko wa Naibu Raisi wa Baraza hilo, Sheikh Ali al-Khatib, ili kujadili vita vya uvamizi wa Wazayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kuchukua msimamo mwafaka kuhusu hujuma hiyo.
Maoni yako